
#HABARI: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu , Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete, amesema kuwa uwepo wa huduma za Kidijitali zinazotolewa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), kunawasaidia wananchi kupata huduma kwa haraha na wakati.
Waziri Kikwete amebainisha hayo alipofika kwenye Banda la Taasisi hiyo kwenye maonesho maalum kuelekea kilele cha siku ya Wanawake Duniani ambayo Kitaifa yatafanyika jijini Arusha.
Ametumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi mbalimbali kufika kwenye maonesho hayo, na kutembelea Banda la PSSSF ili kupata elimu endelevu itakayowasaidia kufahamu mambo mbalimbali ya Mfuko huko.