Back to top

IGP Sirro awataka wananchi kuendelea kudumisha amani kwenye maeneo yao

08 May 2018
Share

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amewataka wananchi wa Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Ikwiriri mkoani Pwani kuendelea kuidumisha amani iliyopo katika maeneo yao pamoja na kutoruhusu shughuli holela zinazofanywa na watu wenyekutaka kuharibu amani ya nchi.

IGP Sirro amesema hayo wakati akizindua mashindano ya mpira wa miguu hatua ya 16 bora maarufu Sirro Cup 2018 michezo ambayo imelenga kuwakutanisha vijana na kuwaweka pamoja wakazi wa wilaya hizo.

Mapema akizungumza wakati wa uzinduzi huo wa mashindano ya mpira wa miguu yenye kauli mbiu “kibiti salama,jamii salama” Mkuu wa wilaya ya Kibiti Mhe. 

Gullamuhusein Kifu,amesema kuwa, michuano hiyo imekuja wakati muafaka katika wilaya yake kipindi ambacho jamii inahitaji amani na ushirikiano wa pamoja katika kujiletea maendeleo.