Back to top

Kagame amesifu namna China inavyoichukulia Afrika kuwa mshirika.

24 July 2018
Share

Rais wa Rwanda Paul Kagame amesifu namna China inavyoichukulia Afrika kuwa mshirika sawa na kuiita hatua hiyo kuwa ni ya kimapinduzi katika masuala ya uchumi wa kisasa katika ulimwengu wenye mabadiliko makubwa katika sekta za miradi ya maendeleo ya kijamii.

Rais Kagame ameyasema hayo baada ya kusaini mikataba kati ya Rwanda na China na Rais wa China aliyeko ziarani nchini humo Xi Jinping ambapo Rais huyo ndiye Rais wa kwanza wa China kuitembelea Rwanda.