Back to top

Kangi Lugola atoa onyo kwa askari wanaosafirisha bangi Arumeru.

15 February 2019
Share

Waziri wa mambo ya ndani Kangi Lugola amesema serikali itachukua hatua kali za kisheria kwa askari watakaobainika kutumia magari ya Jeshi la polisi kubeba kusafirisha ama kusindikiza dawa za kulevya ikiwemo bangi na mirungi bila kujali cheo au nafasi ya askari waliyohusika kwakuwa kinalitia doa jeshi na kuondoa imani ya wananchi kwa jeshi lao.

Waziri Lugola ametoa kauli hilo wilayani Arumeru wakati akipokea gari aina ya Land rover  la Jeshi la polisi wilaya ya Arumeru inayotajwa kukithiri kwa kilimo cha bangi gari lililotolewa na wadau wa maendeleo shirika la kimataifa linalojihusisha na uhifadhi la nchini Ujerumani anasema tabia hiyo mbali na kukatisha tamaa wananchi pia inawakatisha tamaa wafadhili wanaojitoa kusaidia jeshi hilo  kwa maslahi ya taifa.

Akikabidhi gari hilo Mratibu wa kudhibiti ujangili wa taasisi ya Frunk Furt William Mallya anasema wameamua kusadia Jeshi la polisi ili liweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu hasa katika wilaya hiyo ambayo pia inazungukwa na hifadhi ya taifa ya Arusha litasaidia katika ulinzi wa rasimali za taifa.

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro anasema wamepokea agizo la Waziri wa mambo ya ndani kuhusu matumizi ya magari ya polisi na tayari wameanza juhudi za kufufua magari mengine yaliyoharibika ili jeshi ilo lifanyakazi ya ulinzi kwa uhakika.