Moto ambao chanzo chake hakijajulikana mara moja umeharibu majengo makuu yote katika Kasri la Shuri eneo la Urithi wa Dunia la Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO lililopo mji wa Okinawa kusini mwa Japani.
Idara ya zimamoto katika mji wa Naha, ambao ni makao makuu ya mkoa huo, ilipokea simu ya dharura kuhusiana na moto huo muda mfupi leo Alhamisi.