Back to top

KUANZIA OKTOBA MOSI, USAFIRI WA MABASI SAA 24

29 September 2023
Share

Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi imeruhusu mabasi ya abiria kote nchi kuanza kusafiri saa 24 kuanzia Oktoba Mosi mwaka huu baada ya kujiridhisha uwepo wa usalama wa kutosha kwa abiria katika barabara zote kuu .

"Serikali inatangaza rasmi, kuanza kutolewa kwa ratiba za mabasi ya abiria kusafiri kwa saa 24, kuanzia Oktoba mosi, 2023."Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mh.Jumanne Sagini .


Akitangaza uamuzi huo jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani  Mh.Jumanne Sagini amesema wamiliki wa mabasi wanapaswa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu kwa mujibu wa leseni zao na pia madereva wa mabasi, wanapaswa kuthibitishwa na LATRA kwa mujibu wa miongozi inayotolewa mara kwa mara.

Naibu waziri pia amesema LATRA inatakiw akutoa ratiba ya Saa 24, kwa kushirikisha watoa huduma, na kuhakikisha mfumo wa VTS na kituo cha mawasiliono vinafanya kazi wakati wote (Saa 24).

Naye Mkurugenzi wa Usafiri wa Barabara LATRA SACP Johansen Kahatano amesema kabla ya kutoa ratiba kwa wasafirishaji, watasaini tamko ambalo litakuwa na maelezo mahususi ya mambo ya kufanya.

Miongoni mwa vigezo vilivyowekwa kwa wasafirishaji hao ni madereva kusajiliwa kwenye mifumo ya LATRA, kuwepo kwa mtu mahususi wa kufuatilia magari hayo usiku, taarifa za abiria lazima ziingizwe kwenye mfumo wa tiketi mtandao.