Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imefurahishwa na jitihada zinazofanywa na Umoja wa Mapadre Wazalendo nchini (UWAMATA) Jimbo kuu la Mwanza za kuendeleza sekta ya Mifugo kupitia mradi wa unenepeshaji wa Mifugo ulioanza kufanyika kwenye eneo la Umoja huo lililopo Kata ya Malya Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza.