Back to top

Lugola awaonya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani.

16 May 2019
Share

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Kangi Lugola amewataka watumishi wa taasisi zote zilizoko chini ya wizara hiyo, kufanya kazi kwa kufuata sheria, kanuni na maadili ya utumishi wa umma, kulingana na unyeti na dhamana waliyopewa ya kusimamia amani na usalama wa nchi.

Waziri Lugola ametoa wito huo alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa taasisi zilizoko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Amesema serikali inatambua na inayafanyia kazi matatizo yanayowakabili, lakini wasizigeuze kuwa kichaka cha kukiuka maadili ikiwemo kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Akizungumza katika kikao hicho, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bwana Rajabu Kailima amewataka wafanyakazi kutumia mabaraza yao kujadili matatizo yanayowakabili na namna ya kuyatatua badala ya kulalamika hali inayochangia kupunguza ufanisi kazini.