Back to top

Makatibu nchi SADC wakutana kujadili tofauti za sheria.

21 October 2019
Share

Makatibu wakuu wa wanaoshughulikia sekta za mazigira, maliasili na utalii katika  nchi za kusini mwa Afrika (SADC) wameanza kikao chao kujadili  masuala  mbalimbali yanayohusiana na sekta hizo na kuandaa agenda na mapendekezo  yatakayowasilishwa kwenye mkutano wa mawaziri wa nchi hizo unaoanza unaofanyika tarehe 25/10/2019.
 
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho katibu Mkuu wa wizara ya maliasili na Utalii wa Tanzania Prof Adolf Mkenda amesema pamoja na mambo mengine yanayohusu sekta hizi pia watajadili changamoto ya kutofautina kwa sheria kati ya nchi moja na nyingine jambo  linalosababisha utekelezaji wa baadhi ya majukumu kuwa mgumu.
 
Prof Mkenda amesema  pia wanajadili njia bora zaidi za kuendeleza ushirikiano wa vita dhidi ya ujangili wa wanyamapri na pia  kuangalia namna bora zaidi ya uvunaji endelevu wa rasilimali hiyo utakaokuwa na tija kwa wananchi na nchi husika kwa ujumla.

Kwa upande wake katibu mkuu ofisi ya makamu wa Rais Muungano na mazingira Mhandisi Joseph Barongo amesema kwenye sekta mazingira wanajadili namna ya kuweka mpango endelevu wa utakaoweza kusaidia kukabiliana na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
 
Naye Mkurugenzi wa Idara ya chakula ,kilimo na Malisili kutoka sekretarieti ya nchi za SADC Bw, Domingos Zephania amesema pamoja na  kuwepo kwa mafanikio katika utekelezaji wa mipango na mikakati mbalimbali inayowekwa changamoto bado ni kubwa na kwamba asilimia  kubwa zinatarajiwa kupatiwa ufumbuzi katika kikao hicho.