Back to top

Marufuku makanisa na misikiti kutumika kufanyia kampeni.

26 September 2020
Share

Kamati ya amani nchini imepiga marufuku makanisa na misikiti, kutumika kumfanyia kampeni mgombea yoyote wa chama cha siasa.

Hayo yamezungumzwa leo na Mwenyekiti wa kamati ya amani Alhaji Ally Salum na kusema kuwa sio vyema kwasababu wanawakosea waumini wao na kuwalazimisha kuchagua viongozi ambao wanawataka wao.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya amani Mchungaji Deorge Fupe ameongeza kuwa madhabahu inatumika katika kuhubiri haki na hiyo haki si yamtu mmoja si vyema kufanya hivyo.