Back to top

Mashahidi waanza kutoa ushahidi wao kesi ya Sabaya.

19 July 2021
Share

Kesi ya Sabaya na wenzake wawili inaendelea katika mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Arusha ambapo mashahidi wanaendelea kutoa ushahidi wao.

Katika kesi hiyo ya Jamhuri namba 105, 2021 jumla ya Mashahidi 10 wanatarajiwa kutoa ushahidi wao mbele mahakama hiyo. 

Tayari shahidi wa kwanza Bw. Mohamed Saad ameshaanza kutoa ushahidi wake mbele ya  Hakimu mkazi mwandamizi Odira Amworo .

Katika kesi hiyo wapo Mawakili watatu wa serikali ambao ni Tumaini kweka, Abdala chavula na Baraka mgaya na Kwa upande wa mawakili wa Utetezi wako wanne ambao ni Dancan Ola, Moses Mauna, Silvester Kahunduki na Jaston Jastic.