Back to top

Mkurugenzi Mtendaji wa ITV apewa tuzo ya Malkia wa nguvu 2018.

07 April 2018
Share

Mkurugenzi Mtendaji ITV/Radio One Joyce Mhavile amepewa tuzo ya heshima katika kukuza, kusimamia,kuendeleza na kutetea tansia ya habari hapa nchini.

               Mkurugenzi Mtendaji ITV/Radio One Joyce Mhavile.

"Katika Maisha yetu ambayo Mwenyezi Mungu anatupa kwa upendeleo, kila nafasi unayoipata usiseme hii sio, ukishaanza kuchagua hiki sicho hiki ndicho hutaweza kufikia kile unachokitaka"JoyceMhavile.

Pia amepewa tuzo hiyo kama kioo na mfano wa kuigwa kwa viongozi wanawake wenye uwezo wa hali ya juu kusimamia Tasnia ya habari ndio nchini, na ndio maana akapewa tuzo hiyo ya Malkia wa nguvu mwaka 2018.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ali Hapi akimkabidhi tuzo ya heshima Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio one, Joyce Mhavile katika tuzo ya Malkia wa Nguvu mwaka 2018 aliyopewa leo na Clouds Media Group jijini Dar es Salaam.

Tuzo hiyo ya Malkia wa Nguvu mwaka 2018 imetolewa na Clouds Media Group jijini Dar es Salaam, katika kutambua mchango wa mwanamke mwenye uthubutu na ushawishi.

Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,Ruge Mutahaba (Kushoto) Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio one, Joyce Mhavile(Kulia)Aliyevaa nguo nyekundu na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ali Hapi wakiwa katika hafla ya kutoa tuzo ya Malkia wa Nguvu 2018.

Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio one, Joyce Mhavile alipewa tuzo ya heshima ya Malkia wa Nguvu mwaka 2018.