Back to top

Mtoto wa siku moja atupwa chooni shule ya sekondari Kazima.

18 April 2019
Share

Mtoto anayekadiliwa kuwa na umri wa siku moja ametupwa chooni katika choo cha wasichana katika shule ya sekondari Kazima iliyopo manispaa ya Tabora na kusababisha taharuki kwa walimu na wanafunzi shuleni hapo.
 
 Akizungumza na vyombo vya habari katika eneoa la shule hiyo mara baada ya kuvunja choo hicho mkaguzi msaidizi wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Tabora, Bibi Vaireti Machechu, amekemea tabia ya watu wanaofanya vitendo vya kikatili mkoani humo.
 
Aidha mkuu wa shule hiyo ya sekondari ya Kazima, Bw.Mrisho Kivuluga, amesema kuwa kitendo hicho kinaweza kuwa kimefanywa na wananchi kutoka nje ya shule kutokana na kichanga hicho kuonekana na umri wa kuzaliwa na shuleni hapo utaratibu wa kupima ujauzito wanafunzi wa kike unafanywa kila msimu wa masomo.