Back to top

MWIGULU:Serikali imeboresha ushirikiano wake na viongozi wa dini.

05 April 2018
Share

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Dakta. MWIGULU NCHEMBA amesema Serikali imeboresha ushirikiano wake na viongozi wa dini ili kuwaelimisha waumini wao kuhusiana na kuachana na vitendo viovu.

Amesema hali hiyo inatokana na viongozi hao wa dini kuwa kundi ambalo linasikilizwa sana na jamii na limekuwa kinara wa kuhimiza amani na maadili katika jamii.

Waziri huyo wa Mambo ya Ndani ya Nchi ameitaka jamii kutumai madawati ya jinsia ambayo yapo katika vituo vya polisi katika kuyaibua matukio ya uhalifu.

Mapema Bungeni hapo baadhi ya wabunge walisema vitendo vya udhalilishaji watoto  katika jamii vimekuwa vikikithiri na walitaka kujua hatua zinazofanywa na Serikali kuvidhibiti .