
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 01 Oktoba, 2019 amefanya uteuzi na kuwahamisha vituo vya kazi Wakurugenzi wa Halmashauri za Manispaa na Wilaya, na pia amefanya uteuzi wa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mkuu wa Itifaki (Chief of
Protocal).
Wakurugenzi Watendaji walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
1. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Ndaki Stephano Muhuli kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro. Kabla ya uteuzi huo Bw. Ndaki Stephano Muhuli alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara.
2.Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Rehema Said Bwasi kuwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro. Kabla ya uteuzi huo Bi. Rehema Said Bwasi alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga.
3. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Sheillah Edward Lukuba kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Mkoani Morogoro. Kabla ya uteuzi huo Bi. Sheillah Edward Lukuba alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Mkoani Dar es Salaam.
4.Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Mohamed Mavura kuwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani. Kabla ya uteuzi huo Bw. Mohamed Mavura alikuwa Afisa katika Makao Makuu ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
5.Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Ezekiel Henrick Magehema kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya. Kabla ya uteuzi huo Bw. Ezekiel Henrick Magehema alikuwa Afisa Tarafa wa Malangali Mkoani Iringa.
6.Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Diana Sono Zacharia kuwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama Mkoani Mara. Kabla ya uteuzi huo Bi. Diana Sono Zacharia alikuwa Afisa Tarafa wa Ukerewe Mkoani Mwanza.
7.Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Hanji Godigodi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe. Kabla ya uteuzi huo Bi. Hanji Godigodi alikuwa Afisa Elimu Taaluma wa Mkoa wa Dar es Salaam.
8. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Said H. Magaro kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora.Kabla ya uteuzi huo Bw. Magaro alikuwa Afisa Tarafa wa Msata Mkoani Pwani.
9. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. Hawa Lumuli Mposi kuwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro. Kabla ya Uteuzi huo Bi. Hawa Lumuli Mposi alikuwa Afisa Tarafa wa Ifakara Mkoani Morogoro.
10. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Godwin Justin Chacha kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro. Kabla ya Uteuzi huo Bw. Chacha alikuwa Afisa Tarafa wa Maswa Mkoani Simiyu.
Wakurugenzi Watendaji waliohamishwa vituo vya kazi ni kama ifuatavyo;
1.Mhe. Rais Magufuli amemhamisha aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro na kumpeleka kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi Mkoani Singida.
2.Mhe.Rais Magufuli amemhamisha aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani Bi. Advera Ndebabayo na kumpeleka kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Wilson Mahera Charles kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).Kabla ya uteuzi huo Dkt. Wilson Mahera Charles alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Dkt. Wilson Mahera Charles anachukua nafasi ya Bw. Athuman Kihamia ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amemteua Kanali Wilbert Augustine Ibuge kuwa Balozi na Mkuu wa Itifaki (Chief of Protocal) wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Kanali Ibuge anachukua nafasi ya Mhe. Balozi Grace A. Martin ambaye atapangiwa majukumu mengine ya Kibalozi.
Uteuzi wa viongozi hao unaanza leo tarehe 01 Oktoba, 2019.
Wakati huo huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Kepteni Mstaafu George Huruma Mkuchika amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Wilaya (DAS) wawili kama ifuatavyo;
1.Mhe.Kepteni Mstaafu Mkuchika amemteua Bw. Charangwa Selemani Makwiro kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Mkoani Dar es Salaam. Bw. Makwiro anachukua nafasi ya Bi. Sheillah Edward Lukuba ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro.
2.Mhe.Kepteni Mstaafu Mkuchika amemteua Bw. Thomas Salala kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mtwara. Kabla ya uteuzi huo Bw.Thomas Salala alikuwa Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Uteuzi wa Makatibu Tawala wa Wilaya hao unaanza leo tarehe 01 Oktoba, 2019.