Back to top

Saa chache za kujua mbivu mbichi rufani ya Mbowe na Matiko.

30 November 2018
Share

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es saalam imetupilia mbali pingamizi za serikali ya kutaka rufaa ya Mh Freeman Mbowe na Esther Matiko isisikilizwe na hivyo imeaamuru isikilizwe na hivyo imeamua kusilikiza rufaa hiyo leo saa nane mchana.

Awali Mahakamani hapo Wananchi na wafuasi wa vyama mbalimbali vya upinzani walijitokeza kusikiliza maamuzi ya rufani ya viongozi hao ambapo baadhi yao wamezuiliwa kuingia ndani ya mahakama hiyo.

Kufuatia maamuzi ya kuridhia kusikilizwa kwa rufaani hiyo mahakama hiyo itafanya maamuzi kama hatua ya mahakama ya Kisutu kuwafutia dhamana viongozi hao ni sahihi ama laa.

Jana katika vizimba vya mahakama hiyo upande wa Jamhuri uliwasilisha pingamizi wakitaka rufani ya wakina Mbowe itupwe kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukosewa kwa sheria iliyotumikia kuwasilisha rufani hiyo.

Wakili wa serikali Mkuu, Dkt. Zainabu Mango akiwasilisha hoja za pingamizi hilo alidai vifungu vya sheria walivyotumia kuwasilisha rufaa si sahihi hivyo anaomba rufaa itupwe.

Upande wa warufani ukiongozwa na wakili Peter Kibatala nao ulipinga hoja hiyo na kusema haina mashiko kisheria.