Back to top

SERIKALI: TUNAIMARISHA MIFUMO ILI PENSHENI ILIPWE NDANI YA SIKU 60

26 May 2023
Share

Serikali imesema mifuko ya hifadhi ya jamii inaendelea kuimarisha mifumo ya ndani ya ulipaji wa mafao, ili kuhakikisha maombi ya penseni kwa wastaafu wapya yanafanyiwa kazi kwa haraka na kuanza kulipwa, ndani ya kipindi kisichozidi siku 60 kama sheria inavyotaka.
.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe.Patrobas Katambi, wakati akijibu swali, Bungeni Jijini Dodoma, baada ya wabunge kuihoji serikali, kuwa ina mpango gani wa kuhakikisha pensheni za wastaafu zinalipwa kwa wakati kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya ucheleweshaji.