Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tawala za mikoa na serikali a mitaa Mhe.Joseph Kakunda amesema serikali inatambua kupanda kwa gharama za uendeshaji wa shule za umma hasa zile za bweni kulinganisha na fedha ambazo serikali imekuwa ikitoa kwa shule hizo.
Naibu Waziri Kakunda amewaambia maafisa elimu nchini kufuatia serikali kulitambua hilo kwa sasa inafanya utafiti ili kujua gharama halisi ya matumizi ya kila mwanafunzi anapokuwepo shuleni ili fedha ambazo zitakuwa zikipelekwa ziendane na hali halisi.
Amewataka maafisa elimu hao wawe wanawasilisha kwa wakati mapendekezo yao ya nini kifanyike kuboresha sekta ya elimu nchini ili kama mapendekezo hayo ya yanahitaji fedha ziweze kutengwa katika bajeti.
Mkutano huo umehusisha maafisa elimu kutoka nchi nzima ambapo wakati wa ufunguzi ,maafisa elimu hao waliaswa kuifanyia kazi kauli ya Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa ya kuboresha elimu katika shule za sekondari za serikali.
