Back to top

Soko la alizeti ni la uhakika-DC Lindi.

14 August 2019
Share

Mkuu wa wilaya ya Lindi, Bw.Shaibu Ndemanga, amewashauri wakulima wa zao la korosho katika halmashauri ya wilaya ya Lindi pamoja na manispaa ya Lindi, kulima zao la alizeti ambalo zao hilo lina soko la uhakika  na mafuta yake ni mazuri.

Amesema zao la alizeti wakulima wengi kwa mikoa ya Lindi hawalimi zao hilo wengi wamejikita kwenye zao la korosho pamoja na ufuta, wakati kupitia zao hilo wanaweza kujiingizia  kipato kutokana na soko lake kuwa la uhakikia.