Back to top

SPIKA TULIA AKIHUTUBIA MKUTANO MKUU WA IPU BAHRAIN

13 March 2023
Share

Spika wa Bunge la Tanzania na Mwenyekiti wa Kundi la Afrika katika Umoja wa Mabunge Duniani (Africa Geopolitical Group in the IPU), Dkt. Tulia Ackson, leo amehutubia Mkutano wa 146 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ambapo amewasilisha hoja ya dharura kwa niaba ya kundi hilo kuchagiza kuundwa kwa mfuko wa maafa Duniani, kwa ajili ya kusaidia nchi zinazoathiriwa na majanga ya asili, na mabadiliko ya tabianchi.


Akizungumza katika mkutano unaoendelea nchini Bahrain wenye kauli mbiu mkutano huo ni “Kukuza amani na kujenga Jamii Jumuishi yenye kuvumiliana”. Dkt. Tulia pia amezungumzia kuhusu juhudi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Bunge katika kudumisha amani na mahusiano mazuri ya kijamii kwa Wananchi wake pamoja na kuheshimu Maazimio ya Kimataifa katika kulinda na kudumisha amani Duniani.