Back to top

TAKUKURU yatoa tahadhari kwa wagombea wa nafasi za uongozi

22 January 2019
Share

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoani Shinyanga imetoa tahadhari kwa baadhi ya wagombea wa nafasi za uongozi wa serikali za mitaa ambao wameanza kupitapita katika vijiji,mitaa na vitongoji kuomba kura kwa njia isiyo halali hali ambayo inadhaniwa kuwa wameanza kuwarubuni wananchi kwa kutoa rushwa ndogondogo kabla ya wakati wa kampeni kuanza.
 
Kauli hiyo imetolewa na kaimu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga Francis Luena mbele ya waandishi wa habari huku akiwataka watumishi wa umma kuzingatia sheria,maadili na uweledi katika utendaji wao wa kazi na kuwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU kwa lengo la kutokomeza vitemdo vya rushwa nchini.