
Meneja wa TARURA wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma, Mhandisi Oscar Mussa, amesema wametekeleza ujenzi wa madaraja 70 katika mwaka wa fedha wa 2022/2023, huku baadhi yake yakiwa yamekamilika na kuleta tija kwa wananchi.
.
Meneja huyo ameyasema hayo alipotembelea Daraja la Mungaka ambalo ni moja ya madaraja hayo 70, yaliyojengwa katika mwaka wa fedha wa 2022/2023.
.
Aidha, wananchi katika maeneo yalipojengwa madaraja hayo wameishukuru serikali kwa ujenzi huo, wakidai kuwa imewafungulia fursa za kiuchumi ikiwemo kusafirisha mazao kwa gharama nafuu.