Back to top

Tigo Half Marathon 2020 yazinduliwa rasmi mjini Moshi

18 January 2020
Share

Mbio maarufu za Tigo Kili Half Marathon 2020 zimezinduliwa rasmi kimkoa katika viwanja vya Kibo Palace Homes, Mjini Moshi  kwa kushirikisha viongozi mbalimbali, wadhamini, Chama Cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro (KAAA), waandaaji wa mbio hizo na wadau mbalimbali.

Akizindua mbio hizo, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bi. Anna Mghwira aliwapongeza wadhamnini na waandaaji wakiongozwa na Kilimanjaro Premium Lager 42km, Tigo-21km Grand Malt 5km  na wadhamini wengine wa meza za maji kwa kazi nzuri na kusema wamezifanya mbio hizi ziwe maarufu zaidi na pia wameendelea kuutagaza Mkoa wake wa Kilimanjaro. 

Mkuu huyo wa Mkoa aliipongeza kampuni ya Tigo kwa kutoa hamasa kwa watanzania .

“Hii iwe changamoto kuwafanya watanzania wakimbie kwa kasi zaidi ili washinde hata zawadi nyingine kubwa zinazotolewa na waandaaji.

Alitoa wito kwa wafanyabiashara kutumia fursa hii vizuri kwani wakati huu wa Kilimanjaro Marathon ndio muda wa kufanya biashara tofauti tofauti. “Wenye mahoteli anzeni kufikiria kutoa ofa mbalimbali ili washiriki watenge muda zaidi wa kukimbia lakini pia kufanya utalii na wenye mabaa na makampuni mbalimbali mnaweza kuandaa promosheni ya wiki nzima kutangaza biashara zenu 

  
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa  Tigo Kanda ya Kaskazini, Aidan Komba alisema: “Tigo tunajivunia kuwa wadhamini wakuu wa mbio maarufu za Tigo Kili Half Marathon kwa mwaka wa nne mfululizo. 

Tukiongoza sokoni kwenye mageuzi ya maisha ya kidijitali yakiwamo masuala ya fedha, tunafurahi kwa mara nyingine tena kuwezesha usajili na malipo kwa washiriki kwenye mashindano hayo yajayo kupitia kwa huduma zetu kamilifu za fedha - Tigo Pesa. 
 
Alisema kwamba kwa miaka kadhaa sasa, Tigo Pesa imethibitishwa kuwa bora zaidi na mfumo wa kuaminika wa malipo kwa wanariadha wote wenye nia kutoka sehemu yoyote nchini.  “Zaidi ya hapo, tunakaribisha kila mmoja kwa ajili ya kupata kumbukumbu za mashindano hayo na kutumia wengine kupitia mtandao wenye kasi zaidi Tanzania wa 4G+,” akasema.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kili Marathon Race John Addison, kuna mipango ya kusisimua kwa ajili ya mbio hizo za mwaka huu, ikiwa ni pamoja na wikiendi ya sherehe itakayokuwa ikifanyika mjini Moshi, bustani mwanana ya Kilimanjaro Lager kwenye uwanja mbio zitakakomalizikia pamoja na ubunifu mwingine kadhaa kama picha kwa ajili ya njia maalumu kwa kila mshiriki wa marathion na half marathon.

“Washiriki waendelee kujisajili kupitia mtandao na kufanya malipo kwa kutumia credit card kupitia  www.kilimanjaromarathon.com  au kupitia TIGO Pesa -  Piga *149*20# kisha fuata maelekezo,” alisema na kuongeza kwamba washiriki wajisajili mapema ili kuepuka usumbufu kwani usajili utafungwa Februari 7,2019 au nafasi zitakapojaa.