Back to top

Trump kukutana na Kim Jong-un Singapore, Juni 12.

11 May 2018
Share

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kwamba atakutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un Singapore tarehe 12 Juni.

Bw Trump aliushangaza ulimwengu Aprili alipotangaza kwamba amekubali mwaliko wa kukutana moja kwa moja na Bw Kim.

Wawili hao awali walikuwa wamerushiana matusi na vitisho.

Ufanisi huo ulitokea baada ya mazungumzo ya kihistoria kati ya viongozi wa Korea Kaskazini na Korea Kusini.

Trump ametangaza hilo saa chache baada yake kuwakaribisha nyumbani Wamarekani watatu ambao wamekuwa wakizuiliwa na Korea Kaskazini ambao waliachiliwa huru na kuruhusiwa kurejea nyumbani.

Waliachiliwa wakati wa ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo mjini Pyongyang kupanga na kufanya mazungumzo zaidi kuhusu mkutano huo wa Trump na Kim Jong-un.