Back to top

UKAME, MATENGENEZO YA MITAMBO YASABABISHA UPUNGUFU UMEME

22 November 2022
Share

Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) limesema kutokana na ukame mkubwa uliokumba nchi, uwezo wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji umepungua kwa jumla ya megawati 155, huku likibanisha kuwa mtambo wake mmoja wa Kidatu wenye uwezo wa kuzalisha megawati 50 umepata hitilafu na mitambo miwili ya Ubungo III ipo kwenye matengenezo kinga, hivyo kufanya kuwa na jumla ya upungufu wa umeme kwa maji na gesi kuwa kati ya megawati 245 hadi megawati 300.