Back to top

Viongozi wa Korea Kusini na Kaskazini wakutana kwa mazungumzo.

18 September 2018
Share

Rais wa Korea Kusini MOON JAE - IN yuko Korea Kaskazi kwa ajili ya mkutano wake wa tatu na kiongozi mkuu wa nchi hiyo KIM JONG UN.

Rais MOON amesema anadhamiria kuhakikisha kuwa Rais Kim Jong Un anachukua hatua madhubuti za kuondokana na silaha za nyuklia.

Mkutano huo wa viongozi wakuu unakuja wakati kukiwa na mkwamo wa mazungumzo ya kuondokana na silaha za nyuklia kati ya Korea Kaskazini na Marekani.

Kumekuwa na ushahidi kuwa Korea Kaskazini inaendeleza mipango yake ya silaha za nyuklia.

Marekani inaishinikiza Korea Kaskazini ichukue hatua madhubuti za kuachana na mpango wake wa kutengeneza silaha za nyuklia na kuielekeza jumuiya ya kimataifa mahali vilipo vituo vyake vya silaha za nyuklia.

Korea Kaskazini inasisitiza kuwa kabla ya hilo kufanyika, ni lazima ipate azimio rasmi la kumalizika kwa Vita vya Korea pamoja na kuondolewa vikwazo vya kiuchumi.