Back to top

VITUO VINGINE VIWILI VYA MAFUTA VYAFUNGIWA

30 September 2023
Share

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema pamoja na mafuta kuwepo nchini, changamoto ya upungufu wa mafuta katika maeneo mbalimbali ilichangiwa na baadhi ya wamiliki wa vituo kuhodhi mafuta ili kujipatia maslahi ya kibiashara, ikiwemo faida kubwa kutokana na ongezeko la bei za mafuta kinyume na sheria.
.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA,  Bw. Titus Kaguo, wakati akizungumza na waandishi wa Habari, ambapo amebainisha kuwa wamevifungia vituo vingine viwili vya mafuta, kwa muda wa miezi sita, kwa kosa la kuhodhi mafuta, kati ya mwezi Julai na Agosti 2023, huku akivitaja vituo hivyo kuwa ni Rashal Petroleum Ltd, kilichopo Mlimba, mkoani Morogoro na Kimashuku Investment Co. Ltd kilichopo Babati, mkoani Manyara.
.
Aidha, Bw.Kaguo amesema  kila wanapokifungia kituo wanataka umma ufahamu kwa sababu hao ndio wanaochangia kusuasua kwa usambazaji wa mafuta hapa nchini.