Back to top

Wakulima wa korosho wachangia Milioni 600 kuondoa shule za nyasi.

07 May 2018
Share

Kutokana na wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma kukabiliwa na tatizo kubwa la miundombinu ya shule ikiwemo ya kukithiri kwa shule za nyasi, wakulima wa korosho wilayani humo wameamua kuchangia kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni 600 ambazo zimetumika kununua bati 3,132,simenti mifuko 8,720 na nondo 880 kwa lengo la kuondoa kabisa shule za nyasi wilayani humo.
 
Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Bw. Juma homera pamoja na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Tunduru, Bw. Chiza Marando wamesema wakulima hao korosho walichangia fedha zao kupitia mfuko wa elimu ambapo walikubali kukatwa kiasi cha shilingi 30 kwa kila kilo moja ya mauzo ya korosho katika msimu wa 2017/2018 ili kutatua tatizo hilo la miundombinu mibovu ya shule ikiwemo kuondoa kabisa shule za nyasi.

Akizindua mpango wa ugawaji wa vifaa hivyo vya ujenzi,Mkuu wa mkoa wa Ruvuma,Bi. Cristina Mndeme ameagiza ujenzi wa miundombinu ya shule hizo ikiwemo kuondoa shule za nyasi ukamilike ndani ya miezi mitatu huku pia baadhi ya wakulima waliochangia fedha zao wakitoa maoni mbalimbali.