Back to top

Wakulima wa Tumbaku watakiwa kulima mazao mbadala kujikimu kimaisha.

19 October 2019
Share

Wakulima wa Tumbaku nchini wameshauriwa kulima mazao mbadala ili kujikimu kimaisha wakati huu ambao serikali na bodi ya Tumbaku wanaendelea kutafuta ufumbuzi wa kuporomoka kwa soko la zao hilo hali iliyosababisha mlundikano wa Tumbaku kwa wakulima.

Mwenyekiti wa bodi ya Tumbaku nchini, Hassan Wakasuvi, amesema uwezo wa viwanda vilivyopo ni mkubwa lakini uzalishaji bado ni mdogo na kwamba kuporomoka kwa soko hakutokani na mgogoro ulioibuka hivi karibuni baina ya serikali na viwanda vya Tumbaku ambao amedai ulikuwa ni wa ndani ya utawala zaidi ukihusu urejeshwaji wa vat na kesi za tume ya ushindani FCC ambazo serikali inafanyia kazi na uliibuka wakati tayari makisio yalishatolewa.

Kaimu Mkurugenzi mkuu wa bodi ya Tumbaku nchini Stanley Mnozya, akawasisitiza wakulima wa Tumbaku kuzingatia kanuni, sheria na taratibu ya kilimo hicho hasa kuzingatia majiko ya kukaushia kutumia miti badala ya magogo,upandaji wa miti karibu kabisa na mashamba na kutotia uchafu ikiwemo nyuzi ili kuongeza uzito.

Zaidi ya kilo milioni sita za Tumbaku ziko kwa wakulima katika maeneo mbalimbali nchini kutokana na kushindwa kuuzika ingawa jitihada mbalimbali zinafanywa kuhakikisha changamoto hiyo inatatuliwa.