Back to top

WAKUU 2 WA IDARA KIBARUA CHAOTA NYASI NAMTUMBO

18 June 2022
Share

Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma imewasimamisha kazi Afisa Maendeleo ya Jamii Bw.Berens Kamugisha na Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi cha Halmashauri hiyo kutokana na kukiuka taratibu za kazi kwa lengo la kujinufaisha.

Uamuzi wa kuwasimamisha kazi wakuu hao wa idara umetangazwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani cha Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo cha kujadili Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambapo Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Brigedia Balozi Wilbert Ibuge amepigilia msumari wa mwisho katika sakata hilo.