Back to top

WALAZIMISHWA KUNYWA POMBE ZOTE WALIZOIBA.

30 November 2023
Share

Wanaume watatu huko nchini Afrika Kusini wamejikuta katika wakati mgumu baada ya kukutwa wakiiba pombe katika Duka la vinywaji vikali (Pombe) baada ya kulazimishwa kunywa vinywaji vyote walivyoiba kama adhabu yao.

Video ya tukio hilo imesambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwaonyesha wanaume hao watatu wakihangaika kumaliza kunywa pombe zote walizoziiba.

Kulingana na blogu kadhaa za Afrika Kusini na wahusika wa vyombo vya habari vya mtandaoni, kisa hicho kilitokea baada ya wezi hao, takribani watatu, kunaswa na wamiliki wa duka hilo la liqour siku chache baada ya kutengeneza vileo hivyo.

Badala ya kuwapiga au kuwaita polisi, walitumia njia hiyo ya kuwalazimisha wahalifu kunywa pombe walioiba yote.