Back to top

Wananchi wa kijiji cha Mpeta mkoani Kigoma wataka huduma ya maji

13 November 2018
Share

Wananchi wa kijiji cha Mpeta katika kata ya Mganza wilayani Uvinza mkoani Kigoma, wamesema  kijiji hicho chenye karibu wakazi elfu kumi hakina huduma ya maji na hicho wanajikuta wanatumia muda mwingi kutafuta maji.  

Katika kupambana na tatizo hilo shirika la misaada la nchi ya Kuwait limetoa msaada wa kisima huku wakiendelea kuiomba serikali kuwapatia huduma ya uhakika ya maji. 

Kwa upande wake mhandisi wa maji katika wilaya ya Uvinza Matias Mwenda amesema wilaya hiyo inakabiliwa na tatizo kubwa la maji ambapo  ni asilimia 48 tu ya wakazi wake ndio wanaopata maji safi na salama na kwamba kwa kushirikiana na wadau wanaendelea kuboresha huduma hiyo.