Back to top

Wananchi wajitokeza kujenga vyumba vya Madarasa Musoma.

02 August 2018
Share

Maefu ya wananchi ya wananchi wa kata ya Mwisenge katika halmashauri ya manispaa ya Musoma mkoani Mara bila kujali itikadi za kisiasa wamejitokeza kuchimba msingi ya vyumba vya madarasa na ofisi za walimu katika shule ya msingi ya Mtakuja" B"baada ya kubaini upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa umesababisha mrundikanano wa wanafunzi chumba kimoja huku wengine wakilazimika kusomea chini ya miti.

Zoezi hilo kubwa la maendeleo la uchimbaji wa misingi hiyo ya vyumba vya madarasa na ofisi za walimu mbali na kushirikisha maefu ya wananchi wa kata ya Mwisenge pia limehusisha viongozi wakuu wa serikali na kisiasa wa halmashamari ya manispaa ya Musoma.

Naye mstahiki meya wa halmashauri ya manispaa ya Musoma Mhe. Kapt mstaafu William Gumbo,amewaambia wananchi kuwa serikali hajazuia michango ya maendeleo katika maeneo yao bali kilichozuiwa na serikali ni viongozi kulazimishwa michango bila ya kuwashirikisha.