Back to top

WASAKA WACHAWI MBARONI, MKOANI RUKWA

18 November 2022
Share

Watu 173 wa vijiji 17 vya Wilaya ya Kalambo na Nkasi mkoani Rukwa, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kushirikiana na waganga wa kienyeji maarufu kama 'LambaLamba' ambao wamekuwa wakiwatapeli wananchi kwa kuwatoza fedha ili kuagua na kufanya msako wa wachawi, nyumba kwa nyumba na kusababisha migongano na taharuki kwenye jamii.
.
Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, ACP Theopister Mallya amewataka Watendaji Vijiji mkoani humo kuhakikisha Waganga hao wakienyeji hawaendelei na shughuli hizo.