Back to top

WATU 78 WAFARIKI MAJIRA YA BARIDI AFGHANISTAN

20 January 2023
Share

#HABARI:Maafisa wa Serikali ya Taliban wamesema watu 78 wamefariki dunia, katika kipindi cha zaidi ya wiki moja tu, wakati wa majira ya baridi kali nchini Afghanistan, jambo linalouzidisha mgogoro wa kibinadamu nchini humo.

Msemaji wa Taliban, katika Wizara ya usimamizi wa majanga Shafiullah Rahimi amethibitisha na kubainisha kuwa zaidi ya mifugo 75,000 nayo imekufa kutokana na baridi kali.

Rahimi amesema utawala wa Taliban unajaribu kuwasaidia zaidi ya watu milioni moja kote nchini humo na bado wanajaribu kuzifikia familia nyingi zaidi kuzisaidia.