
Mganga mkuu wa serikali, Prof. Tumaini Nagu amewataka watumishi wa Afya kuzingatia maadili katika utoaji wa huduma ikiwemo kutunza siri za wagonjwa.
.
Prof. Nagu amesema hayo akiwa katika ziara ya kukagua utoaji wa huduma katika vituo vya Afya na zahanati kwa ajili ya maandalizi ya uchanjaji wa Polio, mkoani Rukwa.
.
Aidha, Prof. Nagu amewapongeza watumishi wa Zahanati ya Kilimahewa iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kwa juhudi wanazozionyesha katika kuwahudumia wananchi ikiwa ni pamoja na kumgundua mtoto wenye virusi vya Polio.