Back to top

Wawekezaji 38 wajitokeza kuwekeza viwanda vya Dawa.

04 April 2018
Share

Agizo la rais Dkt. John Pombe Magufuli na kutaka wawekezaji wazawa wajitokeze kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya vya Dawa na vifaa tiba nchini limepokelewa kwa mwitiko mkubwa baada ya wawekezaji 38 kutangaza nia ya kuwekeza viwanda hivyo mpango ambao unaanza utekelezaji wake katika kipindi cha wiki mbili zijazo.

Hatua hiyo imejidhirisha katika mkutano wa wawekezaji wenye nia ya kuanzisha viwanda vya Dawa na vifaa tiba ambao umeandaliwa na waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na waziri wa viwanda biashara na uwekezaji Mhe. Charles Mwijage jijini Dar es Salaam na mawaziri hao kuketi kwa pamoja na wawekezaji wazawa ambao wameitikia wito wa utekelezaji wa sera ya Tanzania ya uchumi wa viwanda kuelekea mwaka 2025 na mawaziri hao wakatoa tathimini juu ya mkutano huo.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na watendaji wakuu wa idara ambao zinajikita na masuala ya Dawa za binadamu akiwemo mkurugenzi mkuu wa bohari kuu ya Dawa nchini MSD Bwana  Laurean Rugambwa ambaye amesena ni fursa nyingine nzuri ya kupunguza gharama ya kuagiza dawa na vifaa tiba kutoka nje ya nchi baada ya viwanda hivyo kuanzishwa na kuwasisitiza wawekezaji hao kuzingatiwa viwango vya ubora wa kimataifa huku wawekezaji wakipongeza juhudi za serikali za kusimamia mapinduzi ya viwanda nchini kwa sasa.