Back to top

Waziri Mkuu Mh. Majaliwa awataka Viongozi wa dini kuhimiza Maadili.

31 March 2018
Share

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amesema viongozi wa dini nchini wanamchango mkubwa katika kuhakikisha taifa linakuwa na raia wenye kuheshimu maadili kwa kuwa sasa kuna maadili ya kigeni ambayo ni mabaya yanaletwa nchini kutokana na utandawazi.

Waziri mkuu ameyasema hayo mkoani Dodoma wakati akifungua mkutano mkuu wa baraza la waislamu Tanzania - BAKWATA na kuongeza kuwa ni bora viongozi hao wa dini wakatumia nafasi yao katika kuhimiza maadili katika jamii.

           Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa.
Viongozi wa Dini wakiwa katika mkutano mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania - BAKWATA uliofanyika leo 31 March 2018 mkoani Dodoma.
Viongozi wa Dini wakiwa katika mkutano mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania - BAKWATA uliofanyika leo 31 March 2018 mkoani Dodoma.

Naye Waziri Nchi Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Suleiman Jafo amesema kuna mataifa duniani yalikuwa yakijivunia amani ambayo walikuwa nayo ila kwa sasa zipo katika machafuko ila Tanzania inaweza kuwa na amani ya kudumu kama viongozi wa dini wakitimiza wajibu wao.

Waziri Nchi Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Suleiman Jafo 

Naye Sheikh mkuu wa Tanzania Mufti Abubakar Bin Zubeir amesema BAKWATA daima imekuwa nguzo katika kusimamia maslahi ya waislamu na kuelezea kushangazwa kwake na kuwepo kwa waislamu ambao hawatambui kinachofanywa na BAKWATA.

   Sheikh mkuu wa Tanzania Mufti Abubakar Bin Zubeir