
Na.Semvua Msangi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amesema vyombo vya habari ni kiungo muhimu kati yake na Serikali katika kuhabarisha umma wa Watanzania kwa mambo yanayotendeka nchini na nje ya nchi hivyo wizara yake haitosita kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wanahabari.
Waziri Mulamula ametoa kauli hiyo alipo tenbelea vyombo vya habari vya IPP kujionea namna vinavyofanya shughuli zake za kila siku za kuhabarisha umma, Juni 04, 2021.
Akiwa ameongozana na ujumbe wake pamoja na mwenyeji wake, Mkurugenzi Mtendaji ITV/Radio One Joyce Mhaville, amepata nafasi ya kutembelea yanapo zalishwa magazeti ya Nipashe, The Guardian, East Africa Radio na Televisheni, Capital Radio na Televisheni pamoja na ITV na Radio One ambapo amesifu uwekezaji uliokuwepo.










Pia kuhusu serikali kuharakisha mchakato wa kupatikana kwa sera ya taifa ya Watanzania waishio nje ya nchi (Diaspora) Waziri Mulamula amesema tayari sera hiyo imeshaandaliwa ambayo inajumuishwa kwenye sera ya mambo ya nje.
Aidha amesema ameguswa na kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na ITV akieleza namna watu wanavyo kifuatilia mijini na vijijini, huku akikoshwa pia na vijana wanaoendesha vipindi kwenye vituo hivyo.
