YANGA NA SIMBA KUKUTANA APRILI 20, KWA MKAPA

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imetangaza tarehe ya mchezo, utakaowakutanisha watani wa jadi, Young Africans na klabu ya Simba (Kariakoo Derby).
.
Mchezo huo ambao ulikuwa haujapangiwa tarehe kwenye ratiba iliyofanyiwa maboresho na kutangazwa Februari 2024, sasa utachezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, siku ya Jumamosi, Aprili 20, 2024, saa 11:00 jioni.