Back to top

ZOEZI LA UTOAJI VITAMBULISHO VYA NIDA KIZUNGUMKUTI

02 August 2022
Share

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi, Mkoani Kagera wamelalamikia zoezi la utoaji wa vitambulisho vya taifa kwa wananchi, wanaoishi katika maeneo ya mipaka ya nchi kutotendewa haki kwa kunyimwa namba za vitambulisho vya NIDA kwa madai ya majina yao kufanana na raia wa nchi jirani.

Wakizungumza katika mkutano wa Kikao cha  Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo wamesema wananchi wengi wamenyimwa vitambulisho vya taifa kutokana na sura na majina yao kufananishwa na raia wa mataifa yanayozunguka mkoa huo.

Mkuu wa Wilaya ya Missenyi, Kanali Wilson Sakulo, amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kwamba kero hiyo imesababishwa na watu walikuwa wakiandikisha majina ya wananchi kutoifahamu Jografia ya wilaya hiyo vizuri na kuitaka idara ya uhamiaji kushughulikia tatizo hilo.