Back to top

VIFO 31 VYA EBOLA VYARIPOTIWA DRC, WHO KUTOA CHANJO

19 September 2025
Share

Shirika la Afya Duniani (WHO) limethibitisha visa 48 vya Ebola na vifo 31 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) tangu mlipuko huo kutangazwa mapema mwezi Septemba. 

Huu ni mlipuko wa kwanza wa Ebola nchini humo baada ya takriban miaka mitatu ya utulivu.

WHO imethibitisha kuwa tayari chanjo dhidi ya Ebola imeanza kutolewa kwa wafanyakazi wa afya na watu waliokaribiana na wagonjwa, hususan katika Mkoa wa Kasai ambako visa vingi vimeripotiwa.

Mamlaka za afya za ndani na kimataifa zinaendelea kuchukua hatua za haraka kuzuia kusambaa zaidi kwa virusi hivyo hatari.