Back to top

UJENZI BARABARA YA BAGAMOYO–TANGA NA DARAJA LA PANGANI

29 September 2025
Share

Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kukamilisha ujenzi wa barabara ya Bagamoyo–Saadani–Tanga pamoja na daraja la Mto Pangani lenye urefu wa mita 525, endapo atapewa ridhaa ya kuunda serikali baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Akizungumza leo Jumatatu, Septemba 29, 2025, kwenye Viwanja vya Gombero wilayani Pangani, mkoani Tanga, Dkt. Samia alisema mradi huo utakuwa chachu ya kuufungua zaidi ukanda wa Pwani kiuchumi na kupunguza changamoto za usafiri zinazowakabili wananchi wa Pangani na Bagamoyo.

Amesema utekelezaji wa miradi hiyo tayari umeanza, ambapo ujenzi wa kipande cha barabara ya Tanga–Pangani (km 50) umefikia asilimia 75, kipande cha Pangani–Saadani–Makurunge (km 95) kimefikia asilimia 50, huku ujenzi wa daraja la Mto Pangani na barabara zake unganishi ukiwa umefikia asilimia 62.

Kwa mujibu wa Dkt. Samia, kukamilika kwa barabara na daraja hilo kutarahisisha usafirishaji wa bidhaa, kuongeza fursa za biashara na kuimarisha uchumi wa wananchi wa ukanda wa Pwani.