Back to top

MTUMISHI ALIYEUMIA KAZINI APEWA BAJAJI

24 November 2025
Share

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Hamad Chande, amekabidhi pikipiki ya miguu mitatu kwa mtumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Bw. Elihuruma Rashid, Askari wa Uhifadhi Daraja la Pili ambaye alipata madhara wakati akitekeleza majukumu yake ya kazi.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo leo Novemba 24,2025 Mhe. Chande alisema kuwa pikipiki hiyo itamsaidia Bw. Elihuruma katika shughuli zake za kila siku na kupunguza changamoto za usafiri alizokua akikumbana nazo baada ya kuumia.

Makabidhiano hayo yalifanyika wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri, ambayo ililenga kujifunza, kujionea shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii, pamoja na kujitambulisha katika taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.