Back to top

TMA yasisitiza juu ya Tahadhari iliyotolewa ya uwepo wa mvua kubwa.

02 November 2017
Share

Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania imesisitiza juu ya tahadhali iliyotolewa ya uwepo mvua kubwa katika baadhi ya maeneo ya nchi na kusema ni vema wananchi wakachukua tahadhari hasa wanaoishi mabondeni.

Tabiri ya TMA bado inaonyesha uwepo wa mvua kubwa kwa siku tatu mfululizo kuanzia Novemba 1 mwaka huu na kwamba dalili zote zinaonyesha Dar es Salaam kukubwa na mvua hizo.

TMA imesema ni muhimu tahadhali zikachukuliwa kwa umakini ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza hasa katika mikoa inayotarajiwa kuwa na mvua kubwa kwa siku tatu kuanzia Novemba 1 ambayo ni pamoja na Tanga, Pwani, Dar es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.