Back to top

Makao Makuu ya H/Mashauri ya wilaya ya Bunda kujengwa Kibara.

22 December 2020
Share

Serikali wilayani Bunda mkoani Mara imeamua makao makuu ya halmashauri ya wilaya hiyo yatajengwa eneo la Kibara na siyo vinginevyo.

Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili ametangaza msimamo wa serikali katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo yenye majimbo mawili ya uchaguzi ya Bunda Vijijini na Mwibara.

Akizungumzia uamuzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Bunda Amos Kusaja, amesema ililazimu ipatikane sehemu mojawapo kati ya Nyamuswa au Kibara ya kujenga makao makuu baada ya mvutano ulioibuka kuhusu eneo la ujenzi wa makao makuu ya wilaya.