Back to top

Japan kuipatia Taiwan dozi milioni 1 za AstraZeneca.

13 July 2021
Share

Waziri wa Mambo ya nje wa Japan, Toshimitsu Motegi amesema nchi hiyo inatarajia kutuma msaada wa dozi milioni moja za AstraZeneca ili kukabiliana na COVID-19 na kufanya jumla ya dozi zilizotumwa na Japan kwenda Taiwan mpaka sasa kufikia karibu milioni 3.4, ambapo kampeni ya chanjo imeongeza kasi.

Wizara ya Mambo ya nje ya Taiwan imekaribisha msaada huo wa Japani na kuelezea "urafiki mzuri ulioko kati ya Taiwan na Japan.

Ifahamike tu kwamba msaada wa kwanza wa chanjo ulitolewa mwezi Juni na mwingine mapema mwezi huu.