Back to top

Majaliwa apokea taarifa ya Kamati ya uchunguzi tukio la moto Kariakoo.

27 July 2021
Share

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amepokea taarifa ya Kamati ya uchunguzi wa tukio la moto uliotokea katika soko la kimataifa la Kariakoo tarehe 10 Julai, 2021 jijini Dar es salaam.


Mheshimiwa Majaliwa amepokea taarifa hiyo kutoka kwa mwenyekiti wa Kamati  hayo, CP Liberati Sabas na kuahihidi kuwa serikali itayafanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolkewa na Kamati hiyo.

 
Akizungumza baada ya kuipokea taarifa hiyo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam, Mheshimiwa Majaliwa amewashukuru na amewapongeza wajumbe wa Tume hiyo kwa kazi nzuri iliyofanyika kwa weledi mkubwa.

 
Mheshimiwa Majaliwa amesema ataifikisha taarifa hiyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwani tukio hilo limewagusa watu ndani na nje ya nchi.