Back to top

WATU 27 WACHARAZWA VIBOKO AFGHANISTAN.

15 December 2022
Share

Maafisa wa Taliban kusini mwa Afghanistan, wamewacharaza viboko watu 27 wakiwemo wanawake wawili, kwa madai ya wizi, kufanya mapenzi nje ya ndoa na makosa mengine.

Adhabu hiyo imetolewa kusini katika majimbo ya Helmand na Zabul.

Msemaji wa serikali ya jimbo Mohammad Qasim Riyaz, amesema kwamba wanaumme 20 wamecharazwa viboko hadharani katika uwanja wa michezo katika mji mkuu wa Lashkar Gah ambapo kila mwanaume amepigwa viboko kati ya 35 na 39 .