
Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC) imewataka wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya Jimbo na Kata kuvishirikisha vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi katika masuala ya kiuchaguzi, ambayo wanastahili kushirikishwa ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao.
.
Wito huo umetolewa na Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Thomas Mihayo, wakati akifungua mafunzo kwa wasimamizi hao, yanayofanyika Mjini Iringa, ikiwa ni maandalizi ya Uchaguzi Mdogo wa Madiwani katika kata 14 za Tanzania Bara unaotarajiwa kufanyika Julai 13, 2023.
